Vanessa Mdee Azidi Kupata Mafanikio na Albamu Yake Ya ‘Money Mondays’
Mwanamuziki
wa Bongo fleva Vanessa Mdee amezidi kufanya vizuri na albamu yake ya
‘Money Mondays’ kwani albamu hiyo imetajwa kuwa ndio inaongoza Afrika
Mashariki nzima.
Kupitia
mtandao wa Boomsplay ambao unahusika na upakuaji wa nyimbo kadhaa
umeweka wazi kuwa Albamu hiyo ndio kinara kupitia mitandao yao ya
kijamii ambapo wameandika ujumbe huu:
"Hongera
nyingi sana kwake @vanessamdee kwa kuwa na albamu namba moja kwa mauzo
na kusikilizwa, ukanda wa Afrika Mashariki nzima ! Wewe kama shabiki
wake mkubwa uliyewezesha hili, tunakupa pongezi pia na endelea kuipa
support “Money Mondays” kila siku!”.
Vanessa
Mdee alionyesha kufurahishwa na taarifa hiyo kwani alitumia ukurasa
wake wa Instagram kushukuru mashabiki zake kwa kuweza kupakua wimbo
mpaka kufanya uwe namba moja:
"Thank
you Asante Sana for making #MoneyMondaysTheAlbum the NO 1 ALBUM in East
Africa @mdeemusicofficialmmetishaaaaaa
@boomplaymusic_tz@boomplaymusicke @boomplaymusicngwith over a million
plays/streams. #SwimmingInJesusJuice #BestFansInTheWorld.”