Mimi Mars Awataka Mashabiki Wake Kufuatilia Muziki Wake sio Muonekano.
Mwanadada
kutoka Mdee muziki Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa anawaomba sana
mashabiki wake kufuatilia zaidi muziki wake na sio mwili wake kwa sababu
kipindi cha nyuma alikuwa mnene sana na alikuwa haupendi kabisa mwili
wake lakini kadri siku zilivyozidi kwenda aliona ni bora kuanza kupungua
ili kukaa sawa lakini kitu cha ajabu kuna baadhi ya watu wamekuwa
wakimsema vibaya kuhusu kupungua kwake.
Mimi
Mars anasema kuwa aliamua kupunguza mwili wake ili kujiongezea
kujiamini zaidi lakini pia kwa sababu mwili wake aliokuwa nao hapo awali
alikuwa haumpendezi sana.
"Nilikuwa
sijafurahishwa na nilchokuwa nina kiona , na klikuwa kikininyima
confidence sana,so ilibidi nijitengeneze na kujibadilisha zaidi ili
kuweka kuwa na ile confidence maana hilo ni swla muhimu zaidi katika
industry tuliona yao sasa.
"Najua
wengi hawajafurahishwa sana na , hawajakipenda na wamekuwa
wakilalamika sana lakini is me, ninafanya kile ninachokipenda
mimi,waendelee kuupenda muziki wangu na kuendelea kuusikiliza lakini
mwili wangu waniachie mimi."