Aunty Ezekiel Awataka Watu Waache Kumdharau Mpenzi Wake Kisa Dansa
Muigizaji
wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu zito watu wote ambao
wamekuwa wakimdharau mpenzi wake lakini pia Baba wa mtoto wake Mose
Iyobo kisa ni mchezo shoo.
Aunty
Ezekiel ameweka wazi kuwa hapendezwi na dharau hizo kwani ingawa wao
wanaweza wakawa wanamuona yeye kama Dansa tu lakini yeye anamuona kama
mkurugenzi fulani.
Aunty
alisema amekuwa akifuatilia kwenye mitandao ya kijamii na kuona watu
wakimchukulia poa Iyobo lakini anawaambia tu, yeye kwake anamuona kama
mkurugenzi.
"Waache
kumchukulia poa Moze wangu. Mimi namuona kama mkurugenzi fulani hivi,
wao wakiona mtuanacheza muziki hawajui kama ni kazi, hawathamini na
kuonesha dharau tu mitandaoni”.
Mose
Iyobo ni Dansa maarufu kutoka WCB ambaye kwa muda mrefu ameonekana
kwenye steji na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz akiwa anakata
viuno.
Aunty
Ezekiel na Mose Iyobo walikutana miaka minne iliyopita na mara moja
watu walianza kumponda Aunty kwa kutoka na Mose Iyobo jambo ambalo
hakujali.