Video: Mbunge John Heche na Matiko waripoti Polisi watakiwa kuripoti tena Agosti 14 Mwaka huu, Waongea na Vyombo vya Habari.
Kutoka kushoto wa pili ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini CHADEMA John Heche katikati ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Serengeti CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima CHADEMA Gimbi Masaba anayefuata ni Mbunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko wakitoka kituo cha Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa ajili ya kuripoti kutokana na Tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya Uchochezi na kuhamamsisha kilimo cha Bhangi. |
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Serengeti CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima CHADEMA Gimbi Masaba akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko katika ofisi za Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya hii leo. |
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini CHADEMA John Heche ambaye anatuhumiwa kwa Makosa Mawili likiwemo la Kuruka Dhamana na Kuchochea wananchi akiwa Bungeni kuvamia Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA Uliopo Nyamongo Wilayani Tarime na Esther Matiko mbunge Jimbo la Tarime Mjini anayetuhumiwa kwa kosa la kuchochea wanachi kulima zao la Bhangi wakifafanua jambo. |
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyamwaga CHADEMA Moses Misiwa akifuatia Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini John Heche ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti akifuatia Makamu wake ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya CHADEMA Wilaya ya Itilima Mwisho kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko kipindi wakiongea na Vyombo vya habari katika Ofisi za chama hicho baada ya kutoka kuripoti Polisi. |
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini John Heche akiongea na Vyombo vya habari |
Mbunge Heche akieleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyolinda wabunge |