Rais Magufuli Kufanya Ziara ya siku 3 Nchni Uganda
Rais
John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Uganda
ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo tangu aingie madarakani.
Taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema Rais Magufuli
atawasili nchini humo Novemba 9,2017 na atapokewa na mwenyeji wake, Rais
Yoweri Museveni.
Akiwa nchini humo pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli atashuhudia utiaji saini wa makubaliano mbalimbali.
Pia, atatembelea eneo litakalokuwa kituo cha pamoja cha huduma kati ya Tanzania na Uganda.
Taarifa hiyo imesema Rais Magufuli na mwenyeji wake watazungumza na waandishi wa habari Novemba 10,2017.
Ziara
ya Rais Magufuli inafanyika katika wakati ambapo uhusiano wa mataifa
hayo mawili ukitajwa kuimarika zaidi ikiwemo kuzinduliwa mradi wa ujenzi
wa bomba la kusafirishia mafuta.
Bomba hilo la mafuta ambalo litagharimu Dola 3.5 bilioni za Marekani litapita katika mikoa minane nchini.
Mara ya mwisho Rais Magufuli kutembelea Uganda ilikuwa Mei 2016 alipokwenda kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Museveni.
Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amezitembelea nchi za Kenya, Rwanda na Uganda.
