Mwigulu awataka wananchi kutofanya hasira kwenye kuchagua Madiwani.......Awataka Waichague CCM
Waziri
wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi
CCM Mwigulu Nchemba amewataka wananchi ambao wanafanya uchaguzi mdogo wa
udiwani nchini wasitumie hasira kwenye upigaji kura bali wachague
wagombea wa CCM ili kutimiza nguzo tatu za uongozi.
Mh.
Nchemba ameyasema hayo wakati akimnadi Mgombea udiwani wa kata ya
Nangwa wilaya ya Hanang ambapo amewaambia wananchi watambue kwamba
serikali iliyopo madarakani inaongozwa na CCM hivyo wachague wagombea
hao
Aidha
Mh. Nchemba ameongeza kwamba uchaguzi mdogo ni uchaguzi rahisi sana
kama watu wataamua kutafakari kwasababu ilani inayotekelezwa ni ya CCM
na la pili ni huu ni uchaguzi wakujaza nafasi
"Kwasasa
ilani inayofanya kazi ni ya CCM hivyo msifanye hasira katika kuchagua
kwani huwezi kuwasha tochi kwa kuweka mabetri mawili ya CCM alafu la
tatu liwe bunzi, Tochi haiwezi kuwaka," Mh. Nchemba
Pamoja
na hayo Nchema amewataka wananchi hao waweze kumpitisha mgombea huyo
mwanamke kwa kudai kwamba anafaa kuongoza na kwamba wa kina mama ni
waaminifu zaidi kwani Diwani aliyepita alikuwa mwanaume lakini
alihukumiwa mahakamani kwa kosa la ubadhilifu wa mali za umma
