Hakimu Atoa Onyo.....Atishia Kuifuta Kesi ya Vigogo wa NIDA
Hakimu
Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Respicious Mwijage ameuambia upande
wa mashtaka kuwa siku akipandwa na mashetani ataifuta kesi ya vigogo wa
Mamlaka ya Vitambulisho vyaTaifa (NIDA) endapo kama upelelezi
hautakamilika.
Hakimu
Mwijage alitoa angalizo hilo baada ya Wakili wa Serikali, Peter Vitalis
kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na baada ya kusema
hayo, Hakimu Mwijage alisema kesi hiyo ina takribani siku 365 na
upelelezi haujakamilika jambo ambalo linatoa taswira mbaya.
“Kamilisheni
upelelezi ili kama hawa wamekula fedha za umma wafungwe au kama
hawajala waachiwe huru, siku mashetani yangu yakipanda nitafuta hii
kesi.”
Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi December 6,2017 huku akiutaka upande wa mashtaka kufika na taarifa kuhusu upelelezi.
Kesi
hiyo inamkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa (NIDA), Dickson Maimu na
wenzake saba, ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na
kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 1.16.
Mbali
na Maimu, washtakiwa wengine ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin
Mwakatumbula, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria,
Sabina Raymond, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery
Ndege, Xavery Kayombo, Meneja Biashara wa mamlaka hiyo, Avelin Momburi
na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph
Makani.
Washtakiwa
pamoja na mashtaka mengine yakiwemo kuisababishia Serikali hasara
wanadaiwa tarehe tofauti kati ya January 15 hadi 19, mwaka 2010 katika
Makao Makuu ya NIDA wilayani Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa
watumishi wa umma kwa nafasi walizokuwa nazo walitumia madaraka vibaya
kwa kuidhinisha malipo bila kufuata viwango vya kubadilishia fedha.
