Mdogo wa Tundu Lissu Afunguka Mazito Sakata la Kaka Yake Kupigwa Risasi
Mdogo
wake na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayefahamika kwa jina
la Vicent Lissu Mughwai amefunguka kuhusu sakata la kaka yake kupigwa
risasi na kusema anaumia kwa ajili ya Watanzania.
Mdogo
wake na Tundu Lissu amesema hayo jana alipokuwa kwenye kanisa la Ufufuo
na uzima ambao aliwashukuru Watanzania kwa kumuombea kaka yake huyo
ambaye kwa sasa anaendelea vizuri na kudai kuwa anaamini kupitia yeye
haki ya nchi itapatikana kwani ili haki ipatikane lazima watu wengine
waumie.
"Mimi
ni mdogo wake na Tundu Lissu akitoka yeye kuzaliwa ndiyo mimi nafuata,
baba askofu naanza kukushukuru kwa maombezi maalum kwa ajili ya ndugu
yangu huyu lakini pia nawashukuru Watanzania wote kwa maombezi ndugu
zangu nimekuja hapa kusema kitu kimoja tu ni shukrani kwa sala zenu,
tuko hapa leo ndugu yangu Lissu amelala hospitalini alipigwa risasi
nyingi sana, nilibahatika kwenda siku hiyo hiyo, tulikwenda moja kwa
moja hospitalini Dodoma, madaktari wengi walifanya kazi nzuri sana,
wataalamu wanasema katika matukio kama hayo yale masaa ya mwanzo ni
"very critical" alipigwa risasi nyingi sana na kuvuja damu nyingi"
alisisitiza mdogo wake Tundu Lissu
Mdogo
wake na Tundu Lissu aliendelea kusema kuwa "Tukio hili lilitokea kwenye
sehemu ambayo ni sehemu ya mawaziri, mimi namjua Lissu ni mtu ambaye
anapenda haki sana, toka utotoni, kinachoumiza zaidi mtu ambaye anataka
haki, mtu anayetaka usawa kwa watu wote, mtu anayepigania haki za katiba
leo yupo kitandani na ilikuwa awe amekufa lakini kwa nguvu za Mungu
aliyehai Lissu leo yupo mzima na tunaomba na kushukuru na tunaomba
tuendelee kumuombea ndugu yetu" alisema mdogo wake na Tundu Lissu
Aidha
Mdogo wake na Tundu Lissu amesema kuwa anashangaa kwanini vyombo vya
usalama havikutaka kufanyia kazi taarifa ambayo awali alishaitoa kuhusu
watu ambao wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu ambao alishawahi
kuwasema katika mkutano wake na vyombo vya habari.
"Bahati
mbaya sana watu wanaotetea haki ndiyo wamekuwa wakiumia, ndugu yangu
karibu miezi miwili hivi alikuwa anafuatwa na watu na alitoa taarifa
tena aliongea na vyombo vya habari kuwa nafuatwa kila napokwenda, lakini
ndiyo hivyo tena ila tunaimani kwa nguvu ya Mungu atapona, naomba
nitumie nafasi hii kuwaomba tuendelee kuzidi kumuombe, naamini nchi yetu
itakuwa na amani na haki kwani muda mwingine haki inapatikana baada ya
watu wengine kuumia kama ambavyo ndugu yangu ameumia" alimaliza mdogo
wake na Tundu Lissu
