Zuma kitanzini tena.........Bunge la Afrika Kusini leo litapiga kura ya kutokuwa na imani nae

Wabunge nchini Afrika Kusini leo wanatarajia kupiga kura ya siri ya kuamua kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.

Baleka Mbete ambaye ni spika wa bunge hilo amefikia uamuzi huo mara baada ya vyama vya upinzani kufungua kesi mahakamani wakitaka ipigwe kura ya siri dhidi ya Rais wa nchi hiyo ya kutokuwa na imani naye.

Aidha, Wabunge hao wanaamini kwamba iwapo kura ya siri itapigwa, basi wabunge wa chama tawala cha African National Congress (ANC) ambao wanampinga Zuma watakuwa na uhuru wa kupiga kura dhidi ya rais huyo.

Chama cha ANC, ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Wazungu mwaka 1994, kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge la nchi hiyo.

Hata hivyo, hili ni jaribio la hivi karibuni la kutaka kumuondoa madarakani Rais Zuma na linatokea mara baada ya  kumfukuza kazi waziri wa fedha aliyekuwa anpendwa sana na wabunge wengi, Pravin Gordhan pamoja na mawaziri wengine katika mabadiliko yake kwenye baraza la mawaziri mwezi Machi.
Powered by Blogger.