Rais Museveni abadilisha tarehe yake wa kuzaliwa
Kwa
muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii
nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta
Museveni.
Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena.
Lakini
nadhari nyingine imeibuka ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka
kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo
wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na
hivyo sasa ana miaka 70.
Kwa
minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda
itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena
katika awamu ya sita.
Museveni alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awamu ya tatu.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo, Rais amewahi kusema kwamba hafahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
“Wazazi
wangu hawakwenda shule na hivyo hawakujua tarehe,” alinukuliwa Rais
Museveni mwaka 1997 alipokuwa akitoa taarifa zake katika mahojiano
maalum.
Mkanganyiko
huu umekuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Museveni aliposema
kuwa katika kipindi cha miaka 31 alichokuwa madarakani hajawahi kuugua.
“Umewahi
kusikia Museveni ameumwa na miguu yake kuning’inizwa hospitalini kwa
miaka 31 iliyopita? Hii ni kwa sababu nafuata hatua za msingi za afya
ambazo zimenisaidia kuepukana na magonjwa. Magonjwa haya yanaweza
kuzuilika,” alisema Museveni akitamba kwamba afya yake ni imara.
==>Hapa chini ni nyaraka zake za Ubatizo zilizotolewa na Ikulu ya Uganda.