Wakenya milioni 19 kupiga kura Leo Kuchagua Rais na Viongozi Wengine
Wakenya milioni 19 wanashiriki kwenye uchaguzi wa kihistoria leo
Kiongozi
wa chama tawala cha Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta, anachuana tena na
hasimu wake wa kisiasa, Raila Odinga wa muungano mkuu wa upinzani, NASA,
kwenye kinyang'anyiro kinachotazamiwa kuwa cha vuta ni kuvute baina ya
wawili hao, licha ya kuwepo wagombea wengine saba wa urais.
Uchaguzi
huo unaowagharimu walipakodi wa Kenya shilingi bilioni 49 unaelezwa
kuwa ghali zaidi ikilinganishwa na uchaguzi katika mataifa jirani.
Zaidi
ya wagombea 1,000 watachaguliwa na Wakenya kwenye nafasi za urais,
ugavana, useneta, ubunge, uwakilishi wa akinamama na wa kaunti
mbalimbali.
Kuna
vituo elfu 40,883 vya kupigia kura vitakavyolindwa na maafisa 150,000
wa idara za usalama, na zaidi ya waangalizi 9,000 wa kitaifa na wa
kigeni wameidhinishwa kuangalia uchaguzi huu.