Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wa CUF wamuunga mkono Profesa Lipumba
Wenyeviti
50 wa Serikali za Mitaa wa CUF Mkoa wa Dar es Salaam wametangaza
kuunga mkono uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF la upande wa
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa
Ibrahim Lipumba kuwa vua uanachama wabunge wanne wa viti maalumu na
madiwani wawili.
Wabunge
waliovuliwa uanachama ni Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally,
Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Raisa Abdallah Mussa, Riziki
Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.
Wakiwakilisha
wenzao 36 wenyeviti 14 kutoka mitaa mbalimbali ya halmashauri za
manispaa tano za Dar es Salaam wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya
kuridhisha na kazi nzuri inayofanywa na Profesa Lipumba.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake 14 mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga
B, Shilingi Shilingi amewaambia wanahabari leo Jumanne Agosti 8
wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao
wamebainika kukihujumu chama hicho.
"Tunamtambua
Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake
inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF," amesema Shilingi
Mbali
na hilo Shilingi amewataka watu wanaoingilia mgogoro wa chama hicho
kuacha mara moja na kwamba mgogoro ni wa kikatiba na suala hilo lipo
mahakamani muda si mrefu uamuzi utatolewa.