MWANAUME AFARIKI BAADA YA KUPIGA KURA KENYA
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Patrick Odoyo amepoteza fahamu na
kufariki masaa matano baada ya zoezi la upigaji kura kuanza, katika eneo
la Nyando Kisumu nchini Kenya.
Patrick Odoyo ambaye alikuwa mtu wa tano kupiga kura katika kituo cha
kata ya Kobura, alipoteza fahamu na kisha kukimbizwa kituo cha afya cha
Ahero ambako mauti ilimkuta, na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha
maiti.
Mpaka sasa haijajulikana sababu ya mtu huyo kupoteza fahamu na kufariki,
lakini vyanzo vya habari vimeeleza kuwa watu wengi wametoka nyumbani
alfajiri kuwahi kupiga kura bila kula kitu chochote, na hali mbaya ya
hewa.