Halima Mdee Aimagia Sifa Kenya
Mbunge
wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CHADEMA, Halima Mdee
amefunguka kwa kuwapongeza wananchi wa Kenya kwa kuweza kubadilisha
Katiba ya nchi yao ambapo leo hii imeweza kuwasaidia wafungwa kupiga
kura wakiwa katika magereza yao.
Mdee
amebainisha hayo kupitia ukurasa wake twitter baada ya kuona picha
zilizokuwa zinagaa katika mitandao ya kijamii asubuhi ya leo
zikiwaonyesha baadhi ya wafungwa wa nchi ya Kenya wakiwa wamejipanga
foleni wakisubiri kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura ya kuchagua
viongozi wanaowahitaji.
"Mabadiliko ya Katiba yanavyofanya kazi njema nchini Kenya, Katiba yetu pendekezwa imefungiwa kabatini", ameandika Halima Mdee.
Hata
hivyo suala la wafungwa kupiga kura nchini humo ni mara ya kwanza tokea
kubadilishwa kwa Katiba yao jambo ambalo limewatamanisha watu wengi
kutoka Tanzania nao kutaka wafungwa waliopo kwenye vifungo wapige kura
nao katika chaguzi zijazo.
Kwa
upande mwingine, Uchaguzi wa mwaka huu unashirikisha wapiga kura
takribani milioni 19.6, kukiwa na ongezeko la wapiga kura wapya milioni
5.2 pamoja na kuwepo vituo 40,883 vya kupigia kura na vimefunguliwa
tangu saa 12 alfajiri katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo na
wanatarajiwa kuhitimisha kupiga kura ifikapo saa 11 alasiri.