Waziri Nchemba aliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wasiovaa kofia ngumu
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi
nchini kuwakamata wamiliki wapikipiki ambao watashindwa kuwa na kofia
ngumu za pikipiki maarufu kama bodaboda.
Waziri
Mwigulu ameyaongea hayo akiongea na madareva wa pikipiki wa wilaya ya
shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani mkoani humo,
Waziri Mwigulu amesema Polisi sasa wakiwakamata madereva wa pikipiki
wakiwa hawana kofia ngumu wawaulize mmiliki wa pikipiki ni nani naye
akamatwe aulizwe kwanini hana kafia ngumu awekwe ndani
Waziri
Mwigulu amesema pia kama abiria naye akikataa kuvaa kofia ngumu na
wakati pikipiki ina kofia hizo basi naye akamatwe na dereva pikipiki
achiwe aendelee na biashara kwani kila mtu lazima atimize wajibu wake
hivyo anatoa mwezi mmoja madereva wote wa pikipiki na wamiliki
wahakikishe wanakofia ngumu mbili za pikipiki.
Naye
mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Steven Masele amesema zamani
palikuwa na msugaono mkubwa sana kati ya madereva wa pikipiki na askari
wa jeshi la polisi hali iliyopelekea kutokuwa na mahusiano mazuri kati
yao lakini kwasasa hivi kuna uhusiano mzuri uliojengwa na RPC mpya.
Kamanda
wa polisi mkoa wa shinyanga ACP Simon Haule amesema mafunzo hayo ni
utekelezaji wa maagizo na mkuu wamkoa baada ya wananchi wengi kutojua au
kutokutumia sheria ya matumizi ya barabara hasa katika mzunguko
(roundabout).
Naye
mmoja wa madereva wa pikipiki wilaya ya shinyanga ameeleza kwasasa
changamoto kubwa wanayokutana ni mfumo usiorafiki wa upatika wa leseni
ya udereva hivyo kufanya madereva wengi wapikipiki kutokuwa na leseni
kwani ni zaidi ya miezi sita tangu alipie kupata leseni hiyo. Waziri
Mwigulu amesema anachukua hilo watalifanyia kazi