Tanzania Kufungua Ubalozi nchini Cuba
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais
wa Cuba, Gladys Bejarano na kumhakikishia ufunguzi wa ofi si za ubalozi
wa Tanzania nchini humo.
Amesema
Tanzania inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia,
kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni kati yake na Cuba,
hivyo inatarajia kufungua ubalozi nchini humo ili kurahisisha utendaji
wa kazi za kibalozi.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Majaliwa alikutana na
Bejarano juzi jioni wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi
nchini Cuba. Malengo ya ziara yalikuwa ni kuimarisha na kudumisha
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
“Tunatambua
uhusiano mzuri uliopo kati Tanzania na Cuba, ambao ulikuwepo kuanzia
Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, hivyo lazima tufungue ofisi za ubalozi na tutamleta
balozi wetu hapa,” alieleza Majaliwa.
Pia
Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa ujenzi wa kiwanda cha dawa
za kuulia vijidudu vya malaria pamoja na ufadhili wa masomo ya
udaktari, inaoutoa kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika vyuo
mbalimbali nchini humo.
Aliiomba
serikali hiyo iendelee kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari hao hadi
ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa sababu Serikali ya Tanzania inawahitaji
madaktari bingwa wengi kwani walioko nchini ni wachache.
Kwa
upande wake, Bejarano alimshukuru Waziri Mkuu kwa kufanya ziara nchini
Cuba na alimhakikishia kwamba uhusiano wa serikali yake na Serikali ya
Tanzania utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote
mbili.
Alisema
Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, inafanya
jitihada kubwa za kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi jambo ambalo
ni tofauti na mataifa mengine.
Makamu
huyo wa Rais alisema Serikali ya Cuba itaendelea kushirikiana na
Tanzania katika uboreshaji wa sekta za afya, utamaduni, kilimo, uchumi
na elimu. Kuhusu ombi la kuongeza ufadhili wa shahada ya uzamili kwa
madaktari, alisema amelip