WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA NA UKATILI WA KIJINSIA.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima Dr Kesam Maswagwa aliyeshiriki katika semina hiyo na kusema kuwa ukatili wa kijinsia hukwamisha maendeleo ya kaya na kuzifanya kuwa duni. |
Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
WADAU wa Maendeleo nchini wametakiwa kujikita katika
kukomesha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ili kuwa na taifa
huru kuelekea uchumi wa viwanda kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Wilaya ya itilima mkoani Simiyu bado inakabiliwa na tatizo hilo ambapo matukio hayo yamekuwa hayaripotiwi katika vyombo
vya dola huku katika mpango wa taifa wa serikali wa mwaka 2017/2022 unaonyesha kuwa wanawake wanne kati ya 10
wanafanyiwa ukatili hasa wa kingono.
Akiongea na wadau wa maendeleo wilayani humo Mkurugenzi wa
Kawiye Social Development Foundation (KASODEFO) Ezekiel Kasanga alisema kuwa
tatizo la ukatili wa kijinsia bado lipo katika maeneo mengi nchini na kuwataka
wadau hao kuhakikisha wanapiga vita aina zote za ukatili.
Alisema kuwa dhamira kuu ya jumuiko hilo ilikuwa ni kukutana
kama wadau na kutengeza mtandao wa
pamoja ili kudhibiti ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto huku akitaja kuwa
wilaya ya Itilima bado inakabiliwa na tatizo hilo.
‘’kimsingi tatizo la ukatili katika wilaya ya itilima bado
lipo, katika takwimu za mpango wa serikali kwa mwaka 2017 hadi 2022, serikali
inatumbia kuwa kati ya wanawake kumi wanne kati yao wanafanyiwa ukatili hasa wa
kingono..tunaielimsha jamii kuachana mila na desturi potofu zinazopelekea I ya
wanawake.’’ Alisema Kasanga.
Aliitaka jamii kupokea elimu ili wapate maarifa juu ya
ukatili wa kijinsia na pia washirikiane na vyombo vya serikali katika
kuwafichua na kuchukua hatua kwa wanaofanya ukatili ili kuwa na jamii yenye
usawa.
Akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima Dr. Kesam
Maswagwa alisema kuwa kwa upande wa serikali matatizo ya unyanyasaji na ukatili
wa kijinsia ni kikwazo kwa maendeleo ya familia kwa sababu kaya nyingi zinapofanyiwa
ukatili zinaendelea kuwa duni na kusababisha hata ukuaji wa maendelea kwa taifa
unakuwa duni vilevile.
Maswagwa alisema kuwa ukatili wa kijinsia ni kikwazo kwa
maendeleo kwa sababu kaya nyingi zinazofanyiwa ukatili huo zinakuwa duni na
zinaendelea na uduni,hivyo wadau wajitahidi kushiriki katika mpango mkakati wa
serikali wa kupiga vita ukatili wa kijinsia ifikapo 2022.
Nao wadau wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia ambao walishiriki
katika semina hiyo wanasema kuwaukatili mwingi huanzia majumbani na hufanywa na
ndugu wa karibu, hivyo ni vyema wadau wakashirikiana kuwajengea uelewa wananchi
juu ya kuripoti aina zote za ukatili unaojitokeza katika maeneo yao.
‘’naomba muwashauri kama mtu amepigwa, kaumizwa iliwaende polisi kuchukua poilisi pia
mtuhumiwa akamatwe, ili tushirikiane kupambana na uhalifu wa aina yeyote
ile,..sisi ndiyo tunakaa na jamii na jamii nyingi inayoishi vijijini bado
inaabudu mila ambazo ni za kikatili na wananshindwa kuzilipoti mahali husikam
kupitia huu muunganiko utatuasidia kutokomeza ukatili’’ alisema Nyansato
Mahunguriro amabye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Itilima.
Ukatili mwingi umekuwa ukitokea katika familia kwa
kuwahusisha ndugu wa damu na kuwafanya kushindwa kuripoti ngazi husika kwa
kuona kuwa wataaibishana na badala yake
mtendewa kubaki na athari za kisaikolojia ikiwemo mimba na kuambikizwa magonjwa
ya zinaa.