Taarifa ya serikali kuhusu madai ya raia 16 wa Somalia, Pakistan na Lebanon kukamatwa uwanja wa ndege Dar.
Tarehe
31/07/2017 chombo kimoja cha habari kilitoa taarifa za upotoshaji
kwamba wageni 16 wenye uraia wa Lebanon, Pakistani na Somalia walinaswa
katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) baada
ya kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP).
Taarifa
sahihi za suala hili ni kwamba Tarehe 30107/2017 abiria wanne (4) Raia
wa Taifa la Pakistan waliwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
eha Julius Nyerere (JNlA) na kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP Lounge)
ambapo nyaraka zao za safari zilikaguliwa na Maafisa wa Uhamiaji na
baadae kuruhusiwa kuingia nchini baada ya kujiridhisha kuwa ni halali.
Abiria
hao walikuwa na kibali kinachowaruhusu kutumia ukumbi wa watu mashuhuri
(VIP) kilichotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Utaratibu
uliopo katika matumizi ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP Lounge) JNIA ni
kwamba wageni wote toka nje ya nehi wanaohitaji kutumia ukumbi huo
wanalazirnika kuomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Wizara husika inapojiridhisha
na vigezo vya waombaji,hutoa vibali hivyo.
Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inatoa wito kwa vyombo vya habari
nchini kuandika habari kwa weledi na kuhusisha pande zote zinazohusishwa
katika taarifa zao mbalimbali, ili kuepuka mkanganyiko na upotoshaji
kwa jamii kwa jambo husika.
TAA
ipo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo chochote cha habari
kinachowasiliana nacho kutaka ufafanuzi wajambo fulani, iii waweze
kuandika kwa umakini na ufasaha zaidi.
IMETOLEW ANA:
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VY A NDEGE TANZANIA (TAA)