Makubwa Haya: MWIZI AKUTWA AMELALA FOFOFO KITANDANI KWENYE NYUMBA ALIYOVUNJA
Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa
polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja
kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.
Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36
alivunja na kuingia nyumbani humo mjini Esperence , magharibi mwa
Australia siku ya Ijumaa.
Alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho ,kulingana na maafisa.
Mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani na kumpata mwizi huyo amelala kitandani mwake.
''Alitoka nje na kuwapigia simu polisi
ambao waliwasili na kumkamata mshtakiwa'', alisema sajenti Richard Moore
kutoka polisi ya Esperence .
Mtu huyo alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana amelewa chakari alisema sajenti Moore.
Ameshtakiwa na wizi.