Saida Karoli Adai Kutishiwa Kuuawa......Aahirisha Show zake Kujinusuru
Ikiwa
imepita miezi miwili toka msanii wa nyimbo za asili Tanzania Said
Karoli arudi rasmi kwenye muziki na kuachia kazi zake mbili zilizopata
mafanikio na kuwafikia watu wengi zaidi ameibuka na kudai watu wameanza
kumpiga vita kishirikina na wanataka kumuua
Said
Karoli ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Orugambo' amedai kuwa
ushirikina upo na watu wanampiga vita ili aweze kupotea tena kwenye
muziki kama ilivyotokea kipindi cha nyuma na kudai kuna mtu amelipwa
pesa ili amuuwe kabisa jambo lililopelekea kuahirisha baadhi ya show
zake.
"Huyo
mtu alinielekeza watu kadhaa ambao wamepanga mpango wa kuniua
aliniambia, sasa mimi nimeshalipwa nikuuwe nikuondoe duniani kabisa
yaani kabla ya kufika Mwanza, Geita tena bora hata hizi show zingine
uvunje, kweli ramani aliyonipa nilichoka ikabidi show zingine za Bukoba
tumezivunja tukasema ngoja tutulie kwanza tuone nini kitaendelea" alisema Said Karoli
Saida
Karoli anakiri wazi kuwa suala la ushirikiana lipo na kwake si jambo la
ajabu kumtokea kwani tayari ameshakutana na mambo ya namna hiyo sana na
kudai yeye anamtegemea Mungu na kumuomba Mungu.
