Wananchi Wamwaga Machozi Moto Ukiteketeza Soko Kuu SIDO Jijini Mbeya


Soko
kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO limeungua moto usiku wa kuamkia
leo .Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku ambapo mali za
wafanyabiashara mbalimbali katika soko hilo zimeteketea.



Kwa
upande mwingine wananchi wamesikika wakimwaga machozi ya lawama kwa
Jeshi la Polisi wakilaumu kutoruhusiwa  kusogea eneo la tukio kuokoa
mali zao kwa kuwafyatulia risasi hewani.


Hii
ni mara ya tatu sasa ambapo soko hili liliisha ungua mara mbili
mfululizo kabla ya  kuungua tena kwa mara nyingine  usiku wa kuamkia
leo.
Powered by Blogger.