Serikali yalipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Serikali
imelipongeza shirika la utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuendelea
kurusha matangazo mubashara katika ziara mbalimbali za viongozi hapa
nchini ikiwemo ziara ya Rais wa Jamhuri Misri hapa nchini.
Pongezi
hizo zimetolewa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan muda mfupi mara
baada ya kuagana na Rais wa Misri katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Julius Kambarage Nyerere.
Amesema
kuwa shirika hilo la utangazaji linafanya vizuri ambapo limekuwa
likihakikisha kuwa kila tukio kubwa limekuwa likirushwa mubashara hivyo
kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa wakati muafaka.
“Niwapongeze
sana TBC, kwani tangu jana tumekuwa pamoja kwenye mapokezi mpaka leo
hii tena wakati wa kumuaga, hivyo hongereni sana na nampongeza
mkurugenzi wa TBC kwa kazi nzuri anayoifanya,”amesema Samia Suluhu.
Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) limekuwa likihakikisha linarusha matangazo
mubashara ili kuweza kuifikia jamii moja kwa moja, hivyo kufikisha
ujumbe kwa muda muafaka
