Wizara ya Mambo ya Ndani yakanusha upotoshaji unaohusu 'Kanuni/sheria za Wizara ya Ndani ya Nchi'
SERIKALI imesema itamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote aliyesambaza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasilino ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Christina Mwangosi, ilisema kumekuwapo na taarifa za uongo zinazosambaa
kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha habari kinachosema “kanuni
na sheria za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zitabadilishwa’.
Taarifa hizo, zimeanza zimeanza kusambazwa juzi zikidai kuanzia janana kuendelea kutakuwa kuna kanuni mpya za mawasiliano.
“Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hii,
ni ya uongo na uzushi,haina ukweli wowote na inalenga kuvuruga
wananchi…tunaomba waipuuze.
“Wizara
inatoa onyo kali kwa mtu yeyote aliyeanzisha na wale wanaoendelea
kusambaza taarifa hii,hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaozusha
mambo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Serikali inao mfumo rasmi wa
utoaji wa taarifa kwa kutumia mfumo wa “kielectroniki na hardcopy,’’
ilisema taarifa hiyo.