Mbunge wa Jimbo la Temeke aswekwa rupango
Mbunge
wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa
na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha
muda.
Akithibitisha
kukamatwa kwake leo Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.
Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda wake.
“Askari wa usalama barabarani walipomhoji aliamua kuwapuuza na kuondoka zake,” amesema.
Amesema polisi walimfuatilia na kumkamata na sasa anaendelea kuhojiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.
“Atafikishwa
mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge
haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.