Waziri Mpango akifunga kituo cha GBP kilichopo eneo la Uwanja wa Ndege, Dar
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza
katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar
es Salaam na kuamuru kituo cha Mafuta cha GBP kifungwe hadi hapo
kitakapo funga mashine maalumu za kutolea risiti baada ya kubainika
hakitumii ipasanyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi (EFD)
Dkt.
Mpango amechukua hatua hiyo baada ya kujionea kituo hicho kikiwa na
pampu nne za mafuta lakini kuna mashine moja pekee ya mkononi ya kutolea
risiti jambo linasababisha wateja wao wengi kutopewa risiti na hivyo
kuikosesha Serikali mapato yake na ni kinyume cha sheria za nchi.
“Sasa
nawachukulia hatua ili liwe fundisho kwa wengine wote wanaouza mafuta
nchini bila kufuata taratibu, na nitaanza na wewe, biashara yako isimame
mpaka mashine zifungwe kwenye kituo chote na utekeleze mara moja,”
alisema Dkt. Mpango
Katika
ukaguzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma, Dkt. Mpango amesifu utaratibu
mzuri uliowekwa na kituo hicho kwa kufunga mashine maalumu za kutolea
risiti zilizounganishwa na kila pampu za mafuta kitu ambacho ndicho
Serikali inavitaka vituo vyote vya mafuta vitumie mfumo huo
“Kituo
hiki kimezingatia sheria sheria kwa kufunga mashine kwa kuzingatia
maelekezo ya Serikali na hapa tunauhakika wa kupata fedha za kuwatumikia
wananchi, kinyume kabisa na kituo cha mafuta nilichokifungia, hapa ndio
ningeomba Watanzania wanunue mafutaĆ¢€ aliongeza Dkt. Mpango.
Ameiagiza
Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini
wamiliki wa vituo vya mafuta wanaokiuka maagizo ya Serikali yaliyowataka
wafunge mashine hizo maalumu tangu mwaka uliopita.
Waziri
wa Fedha na Mipango amewageukia wenye vyombo vya moto wanaonunua mafuta
kwenye vituo vya mafuta kote nchini kudai risiti wanapopata huduma ya
kuwekewa mafuta kwenye vituo hivyo ili kuokoa fedha za Serikali
zinazoishia mikononi mwa wajanja wachache wanaokwepa kodi kwa makusudi
na kuikosesha Serikali mapato yake.
Baadhi
ya wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kupitia Waziri wa Fedha na
Mipango wa kufanya ziara za kushitukiza kwenye vituo vya mafuta na
kutaka hatua hiyo iwe endelevu kwa maafisa wengine wa Serikali ili
kukomesha vitendo vya wenye vituo vya mafuta kukwepa kodi ya Serikali.
Katika
siku yake ya kwanza ya ziara za namna hiyo, Julai 10 mwaka huu, Dkt.
Mpango alikifungia kituo cha Mafuta cha Mawenzi kilichoko Kigamboni,
Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa kituo hicho kimefunga mashine
maalumu za kutolea risiti za kielektroniki lakini hazitumiki na kuamuru
kituo hicho kifungwe hadi kitakapo rekebisha kasoro hiyo na kuvionya
vituo vya mafuta vya OilCom kufunga mashine za aina hiyo mara moja.