Halima Mdee: Mapambano yanaendelea
Mbunge
wa Kaw, Halima Mdee baada ya kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni
10 kwa kudaiwa kutoa lugha chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amewashukuru wote waliopaza sauti zao ili haki itendeke kwake
huku akisema mapambano bado yanaendelea.
Halima mdee ametumia ukurasa wake wa Tweeter kutweet shukrani hizo huku akisema mapambano yanaendelea.
Mhe. Halima ametweet
Halima James Mdee @halimamdee
Kwa heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! #Mapambano yanaendelea!
Kwa
heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki
itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! #Mapambano yanaendelea!
Halima
Mdee alidaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika
mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema uliofanyika katika ofisi za
baraza hilo wakati akizungumza na wanahabari.