TRUMP AUNGA MKONO MAKUBALIANO YA KUIWEKEA VIKWAZO URUSI
Ikulu
ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga mkono
makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la
Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.
Imesema
kuwa Rais Donald Trump, anaunga makubaliano yasiopendelea upande wowote
yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.
Afisa
habari wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee-Sanders anasisitiza kuwa,
licha ya hatua hiyo awali white house ilipinga mswada wa uamuzi huo,
japo kuwa kwa sasa inafurahia mswaada wa mwisho uliopitishwa.Putin amekana nchi yake kuhusika kuingilia uchaguzi huo
Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.
Bunge
hilo linatarajiwa kupiga kura hapo kesho siku ya jumanne kupitisha
muswada huo kuwa sheria inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa
hatua za kidplomasia dhidi ya Moscow.
Ikulu
ya white house hata hivyo imekuwa na kauli zinazotofautiana mara baada
ya msimamo wa bunge la Congress katika vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za
Urusi.
Kupitishwa
kwa sheria hiyo na bunge la congress kutamnyima uwezo Rais Trump,
kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.
Urusi imeendelea kupinda shutuma za kuingilia uchaguzi huo.
CHANZO-BBC SWAHIL