Kafulila afunguka mazito baada ya JPM kumshukuru kwa kuibua sakata la IPTL
Baada
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
kumpongeza David Kafulila kwa kuibua sakata la la IPTL lililowahusisha
vigogo kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo wanasiasa na viongozi kutoka
Serikalini.
Kafulila
ambaye alitangaza kukihama chama chake cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na
Chama cha Demokrasia na Maenfdeleo (CHADEMA), amesema kuwa amefurahishwa
na kauli ya Rais Dkt. Magufuli kuhusu hatua alizochukua kuibua kashfa
ya Escrow.
“Nimefurahishwa
kuona mkuu wa nchi ameguswa na kutambua mchango wangu katika vita hii
hatari ya ufisadi wa IPTL/Escrow kwakuwa imekuwa ikilitafuna taifa kwa
muda mrefu sasa,”amesema Kafulila.
Aidha,
amesema kuwa vita hiyo siyo ya kichama hivyo kila Mtanzania anatakiwa
kuunga mkono ili kuweza kutokomeza na kuwakamata wale wote waliohusika
na ufisadi huo ambao umeiliingizia taifa hasara kubwa.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa anatamani kuona hakuna jiwe lianalobaki katika
ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ikwemo waliobeba
mabilioni katika Lumbesa kutoka katika Benki ya Stanbic ambao hawajawahi
kutajwa hadharani.
Akijibu swali kama sakata la Escrow ndilo lililosababisha yeye kushindwa kutetea jimbo lake, Kafulila amesema vita hiyo imemgharimu mambo mengi huku jimbo hilo likiwa ni sehemu moja,
“Jimbo hilo sikushindwa bali nilinyang’anywa baada ya kuibiwa sana ikashindikana. Nilinyang’anywa na rekodi zipo na ninaweza kuzionyesha na ushahidi wa nguvu zilizotumika kuninyang’anya jimbo hazikuwa nguvu za kawaida,” amefunguka Kafulila.
Akizungumza jana na wakazi wa Kata ya Nguruka, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, Rais Magufuli alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki itakayompeleka motoni.
Alisema anatambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli, hivyo anampongeza sana na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyoni.
Aliongeza kuwa wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa mno na Kafulila alisimama kutetea Umma wa Watanzania.
“Wakamtisha wengine hadi kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili sasa, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu kuwatumikia Watanzania,” alisema Rais Magufuli.