Picha : MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA SHINYANGA
Alhamis Julai 20,2017 Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Zainab Telack amekutana na wawekezaji na wafanyabiashara mkoa
wa Shinyanga kwa lengo la kufahamiana na kujadili mambo kadha wa kadha
ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Shinyanga.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wawekezaji na
wafanyabiashara kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho,Telack
alisema huu ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya
Taifa wa miaka mitano 2016/2017 – 2020/2021 wenye dhima ya kujenga
uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya maendeleo ya watu.
“Ili kutimiza malengo ya mpango huu lazima serikali ifanye kazi kwa
ushirikiano wa karibu na sekta binafsi na nyinyi ni sehemu ya sekta
binafsi na ili kudumisha ushirikiano huo serikali imeanzisha mabaraza ya
biashara katika ngazi ya taifa,mikoa na wilaya”,alieleza Telack.
Aidha alisema uwekezaji ni moja ya shughuli zinazochochea kasi ya ukuaji
wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla ambapo hadi sasa
mkoa huo una jumla ya viwanda 81,ambapo viwanda vikubwa ni 18,viwanda
vya kati 9 na vidogo 54.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 31 za matukio wakati wa kikao hicho,Tazama hapa chini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa
kikao chake pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga
leo Alhamis Julai 20,2017.
Wafanyabiashara,wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwahamasisha wafanyabiashara kushirikiana na kupeana fursa mbalimbali
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwahamasisha wafanyabiashara kushirikiana na kupeana fursa mbalimbali
Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy akizungumza katika kikao hicho.
Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy,katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akifuatiwa na katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy,katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akifuatiwa na katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akichangia hoja katika kikao hicho
Wawekezaji na wafanyabiashara wakiwa katika kikao.
Wawekezaji na wafanyabiashara wakiwa katika kikao.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui akizungumza katika kikao hicho
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro aliyehamishiwa mkoa wa Kinondoni akizungumza ukumbini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro aliyehamishiwa mkoa wa Kinondoni akizungumza ukumbini.
Kikao kinaendelea
Wafanyabiashara na wawekezaji wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Kikao kinaendelea
Mkurugenzi wa Hasmukh Group, Kishan Hasmukh akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Hasmukh Group, Kishan Hasmukh akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila (kushoto) na Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza wakiwa katika kikao hicho
Wawekezaji wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini
Mwekezaji Gilitu Nila Makula akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi wa Soud Group,Hilal Soud akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Katibu wa Wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Macelina Lauo akizungumza wakati wa kikao hicho.
Tunafuatilia kinachoendelea....
Mwenyekiti wa waendesha bodaboda manispaa ya Shinyanga Wenceslaus Modest akichangia hoja
Kikao kinaendelea
Mkurugenzi wa SHUWASA Injinia Sylivester Mahole akichangia hoja ukumbini.
Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila akizungumza katika kikao hicho.