RAIS MAGUFULI AWAHIMIZA WAKIMBIZI KURUDI MAKWAO
Jana Julai 19,2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli alianza ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani Kagera, akitokea nyumbani kwake Chato mkoani Geita alikokuwa na
mapumziko mafupi.
Akiwa mkoani Kagera jana, Rais Dkt.Magufuli alifungua barabara ya
lami ya Kagoma-Biharamulo-Lusangu ambayo ni kiunganishi mhimu cha mikoa
ya Kagera, Geita, Mwanza, Kigoma na Shinyanga lakini pia nchi za
Burundi, Rwanda na Burundi na baadaye kuwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Biharamulo.
Ziara hiyo imeendelea tena leo Julai 20,2017 ambapo mapema asubuhi
alimpokea Rais wa nchi jirani ya Burundi, Mhe.Pierre Nkurunzinza na
kufanya naye mazungumzo ya ujirani mwema ikiwemo kufungua milango ya
ushirikiano baina ya nchi zote mbili (Tanzania na Burundi) kwenye
masuala mbalimbali kama vile usalama na biashara.
Baadaye leo mchana Rais Magufuli akiambatana na mgeni wake, Rais
Nkurunzinza, amewahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Ngara, akiwashukuru kwa kumchagua kuwa Rais na kuahidi
kuwatumikia.
Katika mkutano huo, Marais wote wawili wamewahimiza wakimbizi walio
nchini hususani kutoka Burundi kurejea makwao ili wakajenge uchumi wa
taifa lao na kuonya juu ya mashirika ya wakimbizi kuacha kuwahubiria
wakimbizi kwamba Burundi kuna matatizo na badala yake wawahimize kurejea
makwao.