Picha : MGODI WA ACACIA BULYANHULU WALIPA SHILINGI MILIONI 460 YA USHURU WA HUDUMA KWA HALMASHAURI YA MSALALA
Kushoto ni Meneja Mkuu wa
Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama
Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya
ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
(BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa
Shinyanga leo Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya
Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri
ya Msalala.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi
hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho
ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha
miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia
0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi
hicho.
“Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma
kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania
687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri
mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo
mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.
Alisema kutokana na mgawanyo
huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460
(460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226
(226,928,115.76/=.
"Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi
haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi
machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza
makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini",aliongeza Crew.
Katika hatua nyingine Crew alisema tangu
mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi
10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia
ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi
kwa halmashauri husika mwaka 2014.
“Mgodi wetu unaendelea kuwa na
matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji
madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati
wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na
wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika
na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.
Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili
Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono
jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.
“Hiki kiwango cha shilingi milioni 460
tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na
kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza
kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia,
yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za
kijamii”,alieleza Nkurlu.
Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa
halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo
zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha
huduma za afya na miundombinu.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako
chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha
kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi
milioni 760.
“Sisi tumepokea mapato haya kama
tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato
haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa
mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii
inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu,
tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu
itapata mapato mengi zaidi”,aliongeza Berege.
ANGALIA PICHA WAKATI WA ZOEZI LA KUKABIDHI HUNDI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 460
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu
Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya
Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya
Msalala wilayani Kahama leo Jumatano Julai 26,2017 katika ofisi ya Mkuu
wa wilaya ya Kahama.Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni
460 iliyotolewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa ajili ya ushuru wa
Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa
Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili
Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru
wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
(kulia) akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham
Crew wakati wa zoezi la kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi
milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala hundi yenye thamani ya
Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya
Msalala.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala
Simon Berege akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo Kaimu Mweka
Hazina wa halmashauri hiyo Saleh Bugege (kushoto). Wa kwanza kulia ni
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah
Ezra Terry.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala
Simon Berege akizungumza baada ya kupokea hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya
Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog





