Ombi la Msukuma kwa Rais Magufuli
Mbunge
wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) amemtaka Rais Magufuli
kutosikiliza kelele za baadhi ya viongozi hususani wapinzani na kusema
anapaswa kushikilia hapo hapo aliposhikilia kwani anafanya vizuri na
mambo anayotenda yameanza kuonekana.
Msukuma
alisema hayo juzi wakati wa makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na
taasisi ya The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF) na kusema wao
Geita wapo mstari wambele kuhakikisha wanaunga mkono kila jambo ambalo
linafanywa na Rais Magufuli.
"Mhe.
Rais sisi huku Geita tunakuunga mkono na tupo tayari kujitolea hata
bure katika mambo unayofanya katika nchi hii, nakuomba tu usisikilize
zile kelele za watubali wewe fanya kazi kwa ajili ya Watanzania, maana
kuna watu wengine wanasimama bungeni na kuanza kupiga kelele tu, wengine
wanasimama bungeni na kusema eti unajenga uwanja wa ndege Chato,
usiwasikilize na wala kelele zao zisikukatishe tamaa, ukiona kitu
kingine kizuri chochote usiusahau mkoa wa Geita" alisisitiza Msukuma
Mbali
na hilo Msukuma alikuwa na ombi kwa Rais Magufuli pindi wawekezaji
waliokuwa wakisafirisha makinikia kwenda nje ya nchi wakilipa deni hilo
basi awakumbuke watuwa Geita japo kwa barabara za lami kwani barabara
anadai zimekuwa hazina kiwango kizuri na ni mbovu.
"Sahizi
ukizinguka sehemu ukisema tumetoka Geita kidogo tunakuwa na heshima kwa
ajili yako Rais Magufuli, tunakuomba uendelee hivyo hivyo ombi letu
watu wa Geita, mgodi huu hatufadiki nao, kwa kuwa tulipitisha asilimia 6
tunaomba asilimia 1 tubaki nayo, lakini ombi letu la pili tumekusikia
mara nyingi unasema wawekezaji wakubwa wamekuwa na maeneo makubwa maeka
na maeka, tunaomba vijana wako waruhusu wawekezaji wapunguze maeneo ili
vijana wachimbaji wadogo wakachimbe madini," alimalizia Msukuma
Mbali
na hilo Rais Magufuli alimsifu sana mbunge msukuma na kusema hata
bungeni huwa anamsikia anasimamia sana chama chake (CCM) na kusema kuwa
yupo vizuri sana kwa jambo hilo, kwani anawakilisha vizuri sana.