Mafuta yaadimika Tarime baada ya vituo vitano vya kuuzia mafuta kufungwa sasa lita yauzwa sh 3000
Waitara Meng'anyi.
Shirika la Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) limefunga vituo saba vinavyotoa huduma kwa magari mjini
kwa kutoa huduma ya luuza mafuta bila kuwa na mashine za kutolea risti za
(EFD).
Vituo hivyo viwili ni vya kampuni ya
Efco inayomilikiwa na mbunge wa Musoma Mjini Vedustus Mathayo, viwili vya
mfanyabiashara maalufu wilayani hapa Peter Zakaria kimoja Nyamongo na Viwili
vya Mairo.
Meneja TRA mkoa wa Mara Ernest
Nkang'aza alisema vituo vyote ambavyo havina mashine za EFD vitaendelea
kufungwa hadi hapo vitakapotekeleza agizo hilo.
"Hili ni zoezi la nchi nzima
kwa vituo vyoye visivyokuwa na mashine za elektroniki ya kutolea risti za
malipo havitatoa huduma hiyo hadi hapo vitakapoyimiza agizo hilo," alisema
Nkang'aza.
Pia amewatahadhalisha wamiliki wa
vyombo vya moto kutokujiaminisha kupata huduma ya mafuta nchi jirani ya kenya
kwani wanakiuka sheria.
"Kuingia nchi jirani na
kunywesha mafuta magari yao ni kinyume cha sheria hivyo idara ya uhamiaji
wanalifuatilia suala hilo kuwa baini wanaofanya kazi hiyo," alisema.
Zoezi hilo la kufunga vituo hivyo
lilitekelezwa jana mchana majira ya saa nane, hatua ambayo imesababisha ukosefu
wa mafuta na kusababisha kupanda kwa nauli mara mbili ya nauli ya kawaida.
Wakizungumza na CLEO24NEWS wamiliki wa magari na madereva walisema kuwa
imewalazimu kwenda kutafuta nishati hiyo nchi jirani ya Kenya.
Mwita Mseti anayefanya safari zake
Tarime Musoma alisema kuwa ilimzamu kuwenda kutafuta nishati hiyo mpakani
Sirari ambapo ni umbali wa kilomita 18 kutoka mjini Tarime ambapo kwa sasa
mafuta yanapatikana.
"Upatikanaji wa mafuta kwa saa
hili moja umekuwa shida kweli, hatujui hapo kesho hali itakuwaje kwani mahitaji
yatakuwa makubwa zaidi," alisema Mseti.
Aidha mtumia usafari wa pikipiki
Amina Abdalla mkazi wa mtaa wa Rebu senta alisema kuwa gharama nauli imepanda
maradufu kuliko ilivyokuwa saa chache zilizopita baada ya kufungwa kwa
vituo vyote saba.
"Pale tulipokuwa tunalipa 1000
imepanda hadi 2000, ukihoji wanadai wanafuata mafuta Sirari," alisema
Abdalla.
Muuzaji wa rejareja wa mafuta
ya peterol Dickson Daudi alisema kwa sasa lita moja ni sh,3000 .
"Nilikuwa na akiba nyumbani na
hapa ndipo ninapata faida kwani leo asubuhi (jana) nilikuwa nauza sh,2500 kwa
lita lakini kuanzia saa nane tumepandisha bei kuwa sh3000 na hali ikiendelea
hivi kesho tutauza sh 4000 kwa lita," alisema Daudi.