Lowassa Amlilia Waziri wa Usalama Kenya
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia
kifo cha Waziri wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery
aliyefariki ghafla katika hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi
baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.
Meja
Joseph Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi
wa kiafya kabla ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya
Joseph Kinyua amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa
Kenya.
Baada
ya taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema
Nkaissery alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano
"Natuma
salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri
Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa
mfano, Mungu amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa
Joseph
Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka
mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa
Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa
jamii ya Maasai nchini Kenya.