Lissu ataka wote waliopata fedha za Escrow wakamatwe
Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, Tundu Lissu amesema kuwa watu
wote waliopata mgawo wa fedha hizo wakamatwe kwakuwa wameuthibitishia
umma kuwa ni wala rushwa.
Lissu
amesema kuwa kwa sasa hakuna ubishi kuwa watu hao ni wala rushwa na
walitumia madaraka yao vibaya kujipatia fedha hizo na kuwa watu hao ni
sehemu ya mafisadi ambao wamekuwa wakihujumu nchi.
Ameyasema
hayo baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya
awamu ya nne na mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kurudisha
Serikalini kiasi cha shilingi milioni 40.4 za mgawo wa Escrow hali
ambayo imeibua mijadala mingi.
Ngeleja
ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria, juzi alisema kuwa amefikia hatua hiyo ya kuzikabidhi fedha
hizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kujiweka kando na kashfa
hiyo kwakuwa aliyempa ni mtuhumiwa.
“Sheria
inasema kuwa ukikutwa umeiba unakamatwa unafikishwa kwenye vyombo vya
dola ukikutwa na hatia unafungwa na fedha unarudisha, kwa hiyo hawa wote
waliochukua mgawo huo wakamatwe wafikishwe katika vyombo vya dola na
sio kurudisha tu hizo fedha hawa ni wezi,”amesema Lissu
Hata
hivyo, ameongeza kuwa bila kujali nafasi ya watu hao katika jamii
waliopata mgawo huo wanapaswa kwakuwa hata unapokuwa kiongozi wa dini
hupaswi kula rushwa au kuchukua fedha za rushwa.