Kubenea Amvaa Spika wa Bunge, Job Ndugai
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai hatoshi kuendelea na nafasi hiyo ya
kuliongoza bunge kwani amekuwa akiwakandamiza wabunge wa Chadema.
Kubenea
amemtuhumu Spika kuwa hafai kwa sababu pia alishawahi kupata kashfa ya
kumpiga ndugu yake aliyekuwa mgombea mwenzake wa nafasi ya ubunge Jimbo
la Kongwa Mkoani Dodoma.
Ameyasema
hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wapiga kura wake wa kata ya
Manzese Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa
Ndugai alifanya tukio hilo wakati wa kinyang’anyiro cha kura za maoni
ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Simshangai
Ndugai kwa sababu alimchapa ndugu yake, Mgogo mwenzake, leo amewafungia
wabunge wa upinzani akiwemo mbunge jimbo la Kawe, Halima Mdee na Ester
Bulaya kutoshiriki vikao vya Bunge,”amesema Kubenea.
Hata
hivyo, amewataka wapiga kura wake kutoshangaa kwa kukaa kimya bila
mradi katika Manispaa mpya ya Ubungo kwakuwa Manispaa hiyo bado mpya na
kulikuwa mgawanyo wa miradi hiyo