WAHIMIZWA KUFUATA SHERIA ILI KUONDOA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA.
Kushoto
ni Jamali Juma afisa mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za
Mazingira kwa vitendo (LEAT) akifuatiwa na Afisa habari wa LEAT Edina
Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili wakati wa mkutamo wa hadhara wa kijiji cha kibada ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha kibada
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima
kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali
inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na
taratibu hizo.
Hayo yamesemwa
na Afisa mradi wa Mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za
Mazingira Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada kilichopo
kata ya sadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa kwa kuwataka viongozi na
wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe na maendeleo.
Juma alisema
kuwa sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa kufuatwa kwa
ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kichacho lakini pia inajenga imani
na amani ya kijiji.
"Leo hii
usipofuata sheria na taratibu za kijiji lakina utakwazana na viongozi au
wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa sheria zinakuwa
zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977" alisema Juma
Aidha Juma
aliwataka viongozi wa kijiji cha kibada kuitisha mikutano ya hadhara na
kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji kimetoka
kimaendeleo na ipi mikakati ya kimaendeleo kijiji.
"Ukipita vijiji
vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na
matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi
wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za
kijiji"alisema Juma
Lakini Juma
aliwataka wananchi wa kijiji cha kibada kutunza na kuvilinda vyanzo vya
maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili kuboresha
Mazingira ili yarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kulima kilimo
cha kisasa kwa kutumia teknolojia.
"Jamani kuna
njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa kwa mfano unaweza
kuchukua gunia au sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda mbegu za
mboga na kumwagilia maji machafu unayokuwa unayatumia nyumbani kwao na
kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma
Fadinard
yilikwipande,Shauri na Stephano waliitaka serikali kuanga upya sheria za
kilimo cha mboga mboga kilinacholimwa kwenye utongo mnyevumnye au
karibu na vyanzo vya maji kwa akili ya kilimo changu kwa ajili ya
kujiongezea kipato chao.
"Sisi tunalima
kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala hatuleti
madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka yote
tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa
Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za
mambo ya asili au ya kitammaduni"walisema wananchi wa kibada
Kwa upande wake
Afisa habari wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa
vitendo (LEAT) Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa
kijiji cha kibada kuzifuata sheria walizoletewa za kulinda Mazingira na
vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapoa tamko liingine kuhusu hiyo
sheria.
"Jamani sheria
ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa nguvuni
na kupelekwa mahakama hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi yenu na
kupelekea Msumbufu kwa familia zenu,Mimi nawaomba tiini sheria bila
shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka
Tibaijuka
aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kupelekea
malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili
kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo la sheria hiyo mpya iliyokuja
baada makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu
la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.
Naye Mwenyekiti
wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa serikali
kuifikiria upya sheria waliyoitunga juu ya matumizi ya vyanzo vya maji
kwa kuangalia utamaduni wa watu Vijijini hasa kwenye swala la Kilimo cha
kipindi cha kiangazi maeneo ya mabondeni kwa kuwa wananchi wa Vijijini
wantegemea kilimo hicho.
"Hivi kama huku
wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima kwenye mabonde
maarufu kama Kilimo cha kwenye vinyungu kwa kupanda mboga mboga pamoja
na mahindi ya msimu wa kiangazi"alisema Nyavili