Siku
chache baada ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kuingia
mkataba wa miaka mitano, taarifa zinaeleza sasa mkataba huo utaboreshwa
zaidi.
Taarifa
za uhakika tokea ndani ya Simba zimeeleza mkataba huo utaboresha kutoka
kitita cha Sh milioni 888 kwa mwaka hadi Sh milioni 950.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, awali mkataba walioingia
Simba ulikuwa ni Sh bilioni 4.9 kwa miaka mitano lakini sasa mkataba huo
utakuwa ni Sh bilioni .
“Ni
kweli kabisa, mkataba tulioingia mwanzo sasa umeboreshwa kutoka Sh
bilioni 4.9 kwa miaka yote mitano hadi Sh bilioni 5.173,” kilieleza
chanzo cha uhakika.
“Unajua
wale jamaa wa SportPesa ni waelewa sana, mkataba huu baada ya
kuboreshwa utakuwa sawa kwa sawa kabisa na watni wetu Yanga.”
Taarifa
zimeeleza kwamba Yanga na SportPesa wanaingia mkataba huo rasmi leo na
utakuwa ni sawa kabisa na huo wa Simba baada ya kuboreshwa.
Yanga pia watalipwa Sh bilioni 5.173 kwa mwaka na kufanya timu hizo ziwe zinalipwa sawa kila kitu.
Hivi
karibuni baada ya Simba kusaini mkataba mpya kulizuka tafrani hadi
Zacharia Hans Poppe akatangaza kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji na
uenyekiti wa kamati ya usajili.
Hata hivyo, baadaye Hans Poppe alizungumza na viongozi wa Simba waliomuomba arejee tena.
Kumekuwa
na taarifa viongozi hao pia kuzungumza na Mohamed Dewji ambaye pia
aliamua kujiweka kando akiwa na madai sawa na yake ya Hans Poppe,
kutoshirikishwa.