Wakurugenzi wajadili upatikanaji wa maji Morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mpanda Rojas John Lomuli akiahidi
kuitikia wito wa kuendeleza usafi wa mazingira ili kuhakikisha halamashauri
yake inafikia kiwango cha juu katika utekelezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha
wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro
Mkurugenzi wa
halmashauri ya kondoa Khalifa Kondo akionyesha ishara ya kampeni ya Nipo Tayari ya kutekeleza usafi wa
mazingira katika mji wake wakati wa semina ya kwa wakurungenzi wa halamashauri
nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi mkoani
Singida Rustika Turuka akielezea matarajio yake wakati wa semina ya utekerezaji
wa kampeni ya Nipo Tayari
iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa
matokeo, inayofanyika mjini Morogoro
Sonda Sondacom
Usimamizi
usiofaa wa miradi mbalimbali ya maji nchini umeelezwa kuwa ni kikwazo
kwa juhudi za kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kila familia.
Hayo yalisemwa
jana na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia
Jackson Mutazamba katika semina ya inayofanyika mjini Morogoro
ikijuimuisha wakurugenzi kutoka halmashauri zote nchini.
Alisema lengo
la semina hiyo ni kuweza kuwahimiza na kuwajengea uelewa zaidi
wakurugenzi hawa namna ya kufanya miradi ya maji iweze kuwa na tija na
kufanya upatikanaji wa maji kwa wananchi isiwe kikwazo.
"Utawala bora
katika usimamizi wa miradi ya maji ni kitu cha msingi sana katika
kufanya miradi ya maji iwe endelevu mara baada ya kuanzishwa na kuweza
kuwapatia wananchi maji wakati wote wa mwaka," alisema.
Alisema hadi
mwezi wa tatu mwaka huu mtandao wa maji ulikuwa umefikia asilimia 72
nchini pote lakini miradi mingine haifanyi kazi kutokana na utawala
mbovu hivyo kufanya kuwe na upungufu mkubwa wa maji.
Alisema
wakurugenzi wa wilaya ni viungo muhimu sana katika kufanya miradi hii ya
maji iwe endelevu ukizingatia kuwa serikali na wadau wa maendeleo
wamekuwa karibu sana katika kuhakikisha miradi mingi ya maji
inaanzishwa.
Pia wakurugenzi
wanaweza kusimamia uanzishwaji wa kamati maalumu za maji ambazo
zinasimamiwa moja kwa moja na wananchi wenyewe hivyo kufanya miradi hii
iwe endelevu.
Akiwasilisha
makadirio ya bajeti kwa mwaka 2017/18 bungeni Dodoma wiki iliyopita,
Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwenge alisema
serikali imejipanga kuanzisha miradi mipya mingi ili kuweza kuongeza
mtandao wa maji kufikia asilimia 95.