Si vibaya ukisema wamekubali kiana!
Maana
kipigo cha mabao 2-1 walichokitoa Yanga kwa Mbeya City kinawafanya
wabakize ushindi wa mechi moja tu kubeba ubingwa na kesho wanacheza
dhidi ya Toto African jijini Dar es Salaam.
Watani
wao Simba sasa wanaonekana kukubali kwamba hawana ujanja wa kuwazuia
Yanga ambao ni mabingwa watetezi kubeba tena ubingwa.
Kama
Yanga wakiutwaa ubingwa msimu huu, maana yake ni kwamba watakuwa
wameutwaa kwa mara ya tatu mfululizo, na kuleta tafsiri kwamba
wametawala soka la Tanzania kwa sasa.
Yanga
ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuichapa Mbeya City
mabao 2-1. Imefikisha pointi 65 sawa na Simba lakini imebakiza michezo
miwili wakati Msimbazi wamebakiza mchezo mmoja.
Kwa
michezo ambayo Yanga imebakiza dhidi ya Toto na Mbao, hata kama
itapoteza mchezo mmojawapo, halafu ikashinda mwingine, na Simba kupewa
pointi tatu za mezani ilizopanga kuzifukuzia Fifa, Yanga bado watakuwa
mabingwa kwa kuwa wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kama
kwa vyovyote vile wakilingana pointi, Simba italazimika ishinde mabao
kuanzia 11-0 katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui jijini Dar.
Yanga
ambayo juzi Jumamosi iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya
City, kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 65
sawa na Simba, lakini ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kesho
Jumanne, Yanga itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar,
na kama ikiibuka na ushindi, basi itatangaza ubingwa kwani itakuwa
imeiacha Simba kwa pointi tatu nyuma, huku timu zote zikibakiwa na
mchezo mmojammoja.
Mayanja amesema walikuwa
wakisubiri kuona Yanga wakiteleza mbele ya Mbeya City, lakini matokeo
ya ushindi waliyoyapata yanawafanya kuamini kwamba wapinzani wao hao
wanaenda kuwa mabingwa.
“Tukizungumzia
kiufundi na kuacha ushabiki, Yanga wanaenda kuwa mabingwa wapya wa ligi
kuu msimu huu kutokana na hali halisi ilivyo.
“Ukiangalia
sisi tunashinda, wao wakija pia wanashinda na kukaa juu yetu na
wanabebwa na mabao, hivyo kama mpaka mwisho wa ligi ikiwa hivi unadhani
nani atakuwa bingwa kama siyo Yanga?
“Kuteleza
kwenye mechi kupo, sasa hivi tunasubiri kuona wakipata matokeo angalau
ya sare kwenye mechi zao mbili dhidi ya Toto na Ndanda halafu sisi
tushinde mchezo wetu wa mwisho, hapo ndiyo tunaweza kuwa mabingwa.
“Lakini
hata wakifungwa mechi moja na moja wakishinda, basi mchezo wa mwisho
sisi itatulazimu kufunga mabao zaidi ya kumi kitu ambacho ni kigumu sana
kutokea, hivyo hatutakuwa na jinsi, acha wawe mabingwa tu,” alisema
Mayanja.
Mara
ya mwisho kwa Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilikuwa ni msimu wa
2011/12 na hawajashiriki michuano ya kimataifa kwa zaidi ya miaka
minne. Hata hivyo, wana nafasi ya kushiriki michuano hiyo safari hii
kama watatwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa kuifunga Mbao.