Waitara Meng'anyi,
Mkazi mmoja wa mtaa wa Rebu kata ya Turwa Wilayani Tarime,
aliyefahamika kwa jina la Mniko Marwa (31) anashikiliwa na polisi
katika kituo cha kati mjini Tarime kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka
10 mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Buguti mjini hapa.
Kamanda wa mkoa wa polisi Tarime/Rorya hakupatikana kwa haraka kulizungumzia suala hili licha ya kuwa mikononi mwa jeshi hilo.
Mtuhumiwa
huyo ambaye aliajiriwa kwa kuchimba shimo la choo (sink) na mlezi wa
mtoto huyo Joel Ryoba ambapo alitumia mwanya wa kumrubuni mtoto huyo kwa
kumpa sh,500 siku ya Ijumaa na kutekeleza ubakaji wake kisha kurudia
kitendo hicho jana jumamosi kwa kumpa sh, 500.
Wakati
akitekeleza huo uovu mtoto mdogo aitwaye Wambura Joel (6) aliwaona
wakiingia kwenye boma la nyumba majira ya saa 2:00 asubuhi ambapo wazazi
wao walikuwa wameenda kwenye shughuli za utafutaji ambapo baada ya
kurudi alimweleza mama yake Paskaria Joel.
Baada
ya kuhoji mtoto na kujiridhisha kuwa alitendewa tendo hilo walezi hao
waliamua kumngoja fundi huyo jana asubuhi (leo jumapili) ili aje
kuendelea na kazi yake ambapo alipofika walimweka chini ya ulinzi
kumhoji ambapo alikubali kutekeleza ubakaji huo.
Kufuatia
hatua hiyo ya kukubalia wanamtaa waliazimia kumchape viboko 30 kama
adhabu yake kisha yaishe lakini mbakaji aligoma akionyesha kuwa
anaonewa, ndipo walipoamua kumpeleka kituo cha polisi huku akishambuliwa
kwa fimbo.
Mlezi asimilia
Usiku
wa saa mbili wa siku ya jumamosi nilirudi nyumbani nikauta nyumbani
kwangu kuna hali isiyokuwa ya kawaida na nilipoulizwa waliniambia mtoto
amebakwa na fundi wa kuchimba shimo la choo , baada ya kupata maelezo
hayo nilianza kuuliza wengine ndipo mwanangu wa miaka 11 alisema
alivutiwa ndani ya chumba akapiga kelele akaachiwa, alisema Ryoba ambaye
ni mlezi wake.
Alisema
kuwa aliwashauri wanafamilia hao kumsubiri fundi huyo kwani alikuwa
anakuja kesho yake (Jumapili) ambapo saa mbili asubuhi alifika kazini
hapo ili kukamilisha uchimbaji wa shimo hilo ndipo tukaweka chini na
ulinzi na kuanza kumhoji akakubali kuwa alifanya hivyo kwa makubaliano
na mtoto.
Tulimtaka
tuyamalize kwa kumchapa viboko 30 lakini amekataa hivyo tumeamua
kumfunga kamba kumpeleka kituoni lakini tukiwa njiani tumekutana na gari
la jeshi la polisi wakamchukua na kumleta kituoni ambapo sasa
tumeandika maelezo na kupewa timu namba tatu kwenda hospitalini.
Alisema kuwa mtoto huyo ana mwezi mmoja tangu achukue kutokana kwao kutokana na kuishi katika mazingira magumu.
"Mama
yake alifariki siku nyingi akamwacha anaishi na baba yake ambaye hata
hivyo hana uwezo wa kumhudumia, mtoto alikuwa analala chini kwenye vumbi
chakula ni shida na muda mwingi alionekana na mwanangu wa kike
wanayesoma darasa moja hivyo nikaamua nimchukue aishi kwangu huku
anaendelea kusoma,"alisema.
Anaeleza
kuwa alipomchukua mtoto huyo ilimchukua siku tatu kumpata baba yake
kumwarifu kuwa mtoto wake yupo kwake na tangu hapo anamhudumia kila kitu
kama mtoto wake na hii ndiyo inayonifanya mihangaike kutafuta haki yake
maana hata baba yake hajaonekana kutokana na tabia yake ya kuwa mlevi
kila wakati.
Mtoto aeleza.
Siku
ya Ijumaa alinishika mkono akanioeleka kitandani akanivua nguo mkalalie
naye halafu akanipa sh, 500 ikiwa saa nane mchana, jumamosi saa mbili
alikuja akaniambia akaniambia tuingie kwenye nyumba hiyo mbovu tukalala
naye akanipa sh, 500.
Mtoto
huyo mwenye umri wa miaka 10 na anayesoma darasa la pili shule ya
msingi alikubali kufanya mapenzi na baba wa miaka 31 kwa kupewa sh,500
jambo aliloliita kuwa ni sawa kwake ambapo alitegemea kuitumia kuitumia
shuleni kununua vitumbua.
Mganga athibitisha
Kutokana
na vipimo katika hospitali ya mji wa Tarime vimeonyesha kuwa mtoto huyo
alifanyiwa ubakaji huo kutokana na kuwepo kwa dalili za mahusiano.
Mganga wa zamu ,,,,, alisema kuwa baada ya kufanyika vipimo vya uchunguzi mtoto huyo hakuonekana na magonjwa ambukizi.
Uongozi wa mtaa
Mjumbe
wa mtaa wa Senta Isaya Makoba aliwataka wazazi kuwa waangalifu kwa
watoto wao hasa wanapoondoka kwenda kwenye shughuli za utafutaji ili
kuwalinda wasiweze kukutwa na matatizo kama hayo huku wakiwajengea tabia
ya kukataa vishawishi.
"Tuwajengee
watoto tabia ya kutokuwa wepesi wa kupokea zawadi kwa kurubuniwa ili
kuepusha na madhara ya jinsi hii, na serikali unapobadilika kuwa
mtuhumiwa katende tendo kama hili basi asiwishwe kuhukumiwa ili kutoa
fundisho kwa wengine wenye tabia chafu kama hiki ya Mniko Marwa,"alisema
Makoba.