OMOG ASISITIZA KUHUSIANA NA UWANJA WA JAMHURI NA SUALA LA UBINGWA



Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema kikosi chake kina uwezo wa kutwaa ubingwa katika uwanja wowote.

Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Mbao FC dhidi ya Simba itachezwa Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

“Kwanza Mbao ni timu nzuri, tumecheza nao mara mbili kwenye ligi, tumeshinda mechi zote. Lakini lazima tukubali hii ni mechi ngumu sana.


“Lakini suala la uwanja, kwetu tutaendelea kujiandaa kwa lengo la kushinda au kufanya vizuri,” alisema.
Powered by Blogger.