Tarime.Kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha wananchi wa
kijiji cha Murito Kata ya Kemambo Wilayani Tarime Mkoani Mara wamekumbwa
na maafa ya kuezuliwa Nyumba na baadhi kubomolewa takribani Nyumba 52
zimeezuliwa zikiwemo nyumba 25 za bati.
Mkuu wa wilaya ya Tarime
Glorius Luoga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Maafa wa Wilaya
ametembelea eneo hilo na kuwapa pole wananchi ambao wamekumbwa na tatizo
hilo.
“Nimemwagiza mtendaji wa
kijiji kuorodhesha kwa usahihi nyumba zote za wananchi zilizobomolewa,
na hali ya wananchi hao ambao hawana uwezo kabisa ili niweze kukaa
viongozi wa hata kama tutawaacha hivi hawataweza kupata jinsi ya
kujisaidia kupata pa kujisitili,” alisema Luoga.
Eneo hilo lina
chumvi hivyo miti iliyojenga nyumba hizo zinalika haraka hivyo, hivyo
kuwataka wananchi kupanda miti ya asili ambayo inastawi katika eneo hilo
ili kuweza kuimarisha ulinzi wa nyumba zao.
“Eneo hili halina
miti mingi kutokana na wakazi wake kuwa na mifugo mingi inayoharibu miti
hiyo, ni vyema tukapanda miti ili kusaidia kuzuia upepo mkali
unaotokea,” alisema Luoga. Maeneo yaliyokumbwa na dhahama hiyo ni
vitongoji vya Moroko Senta, Maabera, Kumichongoma, Kesankwe na Keghati
katika kijiji cha Murito
Diwani wa kata ya Kemambo Rashid
Bugomba alisema watu wanalala nje kutokana na madhara yaliyotokea katika
eneo hilo la Mrito huku akiomba serikali kutoa msaada wa hali na mali.
“Nyumba nyingi zilizoezuliwa na makanisa yameezuliwana na tunaomba
msaada mkubwa wa kibinadamu ili kuwasaidia wananchi hao, kwa uwezo wetu
tutajitahidi kuwasaidia tutakavyoweza lakini pia majirani waendelee
kuwasaidia wenzao,” alisema Bogomba.
Wananchi waliokumbwa na
tatizo hilo waliomba serikali kuwapa msaada wa hali na mali ili wapate
sehemu ya kujihifadhi ambapo mwenyekiti wa kijiji cha Murito alieleza
kuwa hali ni mbaya.
“Jumla ya kaya 52 zimeharibiwa na mvua
iliyoambatana na upepo mkali, na kuwafanya wananchi wangu kulala nje
kwani hawana pa kuishi katika kipindi hiki kwa kuwa hata maghala ya
chakula yaliangushwa na upepo kutokana na kuwa mkubwa,”alisema Zephania
Mahati mwenyekiti wa kijiji cha Murito.
|