GEITA YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.
Baadhi ya wadau wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa kikao cha waandishi wa Habari pamoja na wadau wa Habari Mkoani Geita |
Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya Bathromeo Chilwa na Devota Jesse Kutoka Nelico wakibadilishana mawazo wakati wa Kongamano. |
Askofu wa Kanisa la Mungu wa Bendela Heri ya Bwana Majebele akizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari katika jamii. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akizungumza na waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa Siku hiyo. |
Waandishi na viongozi mbali mbali wakiwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari. |
Waandishi wa
habari Wilayani na Mkoani Geita wametakiwa kuandika habari zenye ubora na
zenye kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.
Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mtendeji wa halmashauri ya
Wilaya ya hiyo Bw Ali Kidwaka wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya
habari yaliyofanyika ki Mkoa mjini Geita
.
Amesema ili
kuleta maendeleo katika Taifa na jamii kwa ujumla waandishi wa habari wanapaswa
kuandika habari zenye ubora na zisizokuwa na upendeleo ambazo zitasaidia kwa
kiasi kikubwa watu kujitambua katika kuleta maendeleo ya Taifa na Jamii kwa
ujumla.
Pia
amewataka kuendeleza ushirikiano na taasisi mbalimbali ili kuweza kuibua changamoto ambazo zitaleta maendeleo.
Kwa upande
wake Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye pia ni mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl
Herman Kapufi amesema kuwa ni vyema kwa waandishi kutumia muda mwingi wa
kujifunza maeneo ambayo kwao bado yanautata pia kuwa wazalendo na kushikamana
kwa pamoja
Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe amempongeza mkuu wa
Wilaya ya Geita Pamoja na wadau wengine kuwa bega kwa bega katika kuwasaidia
waandishi ambao wapo wilayani Geita.
“kauli mbiu ya maadhmisho hayo ni klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa
kuendeleza amani katika jamii” ambapo Kitaifa yameadhimishiwa Jijini Mwanza.