Singida United imedhamiria kuleta
mapinduzi ya soka hapa nchini baada ya klabu hiyo kuendelea kujiimarisha
zaidi kwenye usajili wa wachezaji.
Baada ya kufanikiwa kusajili wachezaji wanne wa kigeni leo
hii uongozi wa klabu hiyo umekamilisha usajili wa mshambuliaji aliyewai
kuitumikia ya Mamelod Sondowns na Super Sport za nchini Afrika ya
Kusini.
Mshambuliaji huyo anaetambulika kwa jina la Nhivi Simbarashe
anakuwa mchezaji wa tano kusajili ndani ya klabu hiyo itakayoongozwa na
kocha mahili Hans van Der Pluijm na msaidizi wake Fredrick Minziro.
Simbarashe pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe
amekuwa na mafanikio makubwa kwenye timu alizochezea ikiwemo kufunga
goli pekee ambalo liliwaondosha TP Mazembe katika ushiriki wa michuano
ya kombe la klabu bingwa barani Afrika wakati akiitumikia timu ya
Mamelod Sondowns.
Uongozi wa Singida United umethibitisha kumpa kandarasi ya
miaka miwili mchezaji huyo akitokea klabu ya Caps United ya nchini
Zimbabwe ambapo baada ya kutokea Afrika Kusini alijiunga na timu hiyo ya
nchini kwake.