ANGALIA PICHA JINSI MAPOROMOKO YA MAWE YALIVYOFUNGA BARABARA NA KUANGUKIA MAGARI TANGA
Jeshi la Polisi mkoani Tanga jana
lilifunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia
eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na
matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la
Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba alisema, maporomoko hayo
yalisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na
maeneo mbalimbali nchini
"Hali ya mvua imeendelea kunyesha na
kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha
ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali
iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..
"Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla
kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri
wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama
wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict
Kwa upande mwingine Kamishna huyo
alisema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia
kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya
usafiri.