TANESCO YATOA OMBI KWA WANANCHI WOTE
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi
kwa ujumla kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme
iliyosababishwa na mvua au sababu nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam
leo Mei 11, 2017, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito
Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na hilo pia wananchi wasifanye
shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.
“Lakini tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko
au mkusasnyiko wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za
haraka.” Alisema.
Dkt. Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha
umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au
alama ikawekwa ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo
hilo wakati mafundi wa TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake
iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo
visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua
kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12,
2017.
Aidha kwa upande wake, mtaalamu wa
masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo, amewahakikishia
wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na hitilafu
zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za
kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na
magari, au miti kuangukia nguzo.
"Naomba nitoe angalizo kwa wateja wetu,
kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani kwako, ni vema ukatoa
taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye taaluma badala ya
kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna utaalamu na
masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."
Naye kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika
kipindi hiki cha mvua kuna athari ndogo ndogo zimetokea kwenye
miundombinu ya TANESCO hususan nguzo za umeme, lakini akatoa hakikisho
kuwa mafundi wa TANESCO wanekuwa wakichukua hatua za haraka kurekebisha
athari katika miundombinu ya umeme pindi tu zinapotokea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt.
Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jijini Dar es Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa
wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au
kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi
hiki cha mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi
Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila
Muhaji.
Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea
Dkt. Mwinuka (kushoto) na Mhandisi Kihiyo, wakati wa mkutano huo leo
Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, akitoaufafanuzi zaidi wa
hatua za kuchukua endapo wateja au wananchi wataona hitlafu ya umeme
kwenye maeneo yanayowazunguka
Mhandisi Kihiyo, (kulia0na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari
Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila
Muhaji (kushoto) na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila
wakijadiliana jambo.
Na K-VIS BLOG/Khalfan Said