TFF YAIKOMBOA YANGA ALGERIA, YATOA MKOPO IKATE TIKETI, SASA INAONDOKA LEO USIKU
Wachezaji wa Yanga wanatarajia kuondoka leo usiku nchini Algeria kurejea nyumbani.
Sasa
wanatarajia kuondoka na ndege ya Emirates badala ya Turkish Airways na
imeelezwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limelazimika kutoa mkopo
kwa klabu hiyo ili kuwakomboa.
Wachezaji
saba na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa walichelewa ndege
jijini Algeria na kulazimika kusubiri hadi Jumanne kesho ndiyo waondoke
na kutua nchini kesho.
Mkwasa alisema wataomba msaada kwa MC Alger waliokwenda kucheza nao na kufungwa mabao 4-0 kwa kuwa hawakuwa na fedha za kutosha.
Lakini msaada huo wa TFF utawafanya warejee haraka nyumbani na si Jumatano tena kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa.