PICHA HARMORAPA AANDIKA HISTORIA MPYA DAR LIVE, APIGA SHOO YA KIBABE
Harmorapa si wa mchezo mchezo! Usiku
wa kuamkia leo Ameandika Historia Mpya ndani ya Uwanja wa Taifa wa
Burudani, nazungumzia Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem baada ya
kudondosha Bonge la Shoo tofauti n a watu walivyokuwa wakimbeza.
Harmorapa ambaye anaonekana kuja kwa speed
kali kwenye game ya Bongo Fleva aliisimamisha Dar Live kwa takribani saa
1 kwa kupiga shoo kubwa kwa mara ya kwanza Jijini Dar es Salaam na
Tanzania kwa Ujumla ambapo alikuwa hajawahi kupata nafasi kama hiyo hapo
awali.
Harmorapa aliwadhihirishia mashabiki wake
kuwa yeye siyo wa kubeza kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa
wakimfikiria. Ngoma yake ya Kiboko ya Mabishoo ilinyanyua mashabiki wote
kwenye viti na kujikuta wakipagawa na kuivamia steji huku kila mmoja
akitaka kucheza ngoma hiyo na Rapa huyo.
Shoo yake ilikuwa ya kibabe huku
akishangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki waliofurika Ukumbini hapo.
Hakika ilikuwa ni Historia kwake na kwa mashabiki wake kumtazama LIVE
kwa mara ya kwanza aki-perform jukwaani tena kwenye shoo kubwa kama ile.
Katika shoo hiyo, alikuwepo mkali wa Bongo
Fleva, Juma Nature, Msaga Sumu na wengine kibao ambao waliangusha
burudani ya aina yake ukumbini hapo.