WAZIRI MAKAMBA AWASILI ARUSHA NA KUTEMBELEA WILAYA YA MERU.
Faida
ya Hifadhi endelevu ya Mazingira. Pichani ni eneo la Ngaresero Wilaya
ya Meru ambapo kuna uhifadhi mzuri wa mazingira. Hata hivyo eneo hilo
limeanza kuvamiwa na wananchi kwa shughuli za kibinadamu na kuhatarisha
uhai wake. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo na kumtaka Bw. Timoth
Leach mmiliki wa Ngaresero Mountain Lodge kufanya ukaguzi wa mazingira
mara moja ili kubaina matumizi sahihi ya rasilimali maji.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Edward Moringe Sokoine.
Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha na alitembelea
msitu wa Enguiki na Lendikinya kisha alizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara.
Na Lulu Mussa